Uongozi wa chuo cha
Maendeleo Malya mkoani Mwanza umesema utaendelea kuaanda mafunzo ya Uongozi na
utawala katika michezo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi wa klabu za
michezo za Wizara na Taasisi za serikali zinazojihusisha na micheoz na kupata wataalamu wenye ueledi
Makamu mkuu wa Chuo cha Mandeleo ya michezo Malya kilichopo wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Salumu Mtumbuka amesema mafunzo ya michezo katika uongozi na utawala ni nyenzo za kuwawezesha viongozi kutimiza majukumu yao bila kuvuka mipaka ya kiongozi
Salum Mtumbuka - Makamu mkuu wa Chuo cha Mandeleo ya michezo Malya
Makamu mwenyekiti wa Utamaduni Sports Klabu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Ester Munyuku anaona mafunzo hayo ni sehemu ya kuimarisha uwezo wa viongozi kuongoza klabu zao.
Ester Munyuku - M/Mkiti Utamaduni Sports Klabu
Naye Mratibu wa michezo wa chuo cha Ualimu Mpwapwa cha Dodoma John Kipalamoto amesema wamekuwa mstari wa mbele katika kuibua vipaji vya vijana nan tayari wanao baadhi ya vijana ambao wamekwenda kufanya majaribio katka timu ya TMA inayshiriki ligi ya Championship.
John Kipalamoto - Mratibu wa michezo wa chuo cha Ualimu Mpwapwa
Kwa upande wake mjumbe kutoka Mamlaka ya viwanja vya ndege Dar es Salaam Neema Makasi ambaye amewakilisha timu ya Uchukuzi Sports Club anasema mafunzo hayo yamemtoa nje ya boksi hivyo anaamini elimu hiyo itawasaidia zaidi katika kusimamia timu kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu kwa kutambua michezo ni afya, ajira na huimarisha mahusiana.
Neema Makasi - Kiongozi wa Uchukuzi Spors Club
Mafunzo hayo ya siku sita katika uongozi na utawala yameandaliwa na uongozi wa chuo cha Maendeleo ya michezo Malya na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa michezo wakiwemo viongozi wa klabu za michezo za Wizara na Taasisi za serikai zinazojihusisha na michezo.
Mwisho
0 Comments