Ticker

6/recent/ticker-posts

WAGOMBEA WATAHADHARISHWA


 


Wagombea ubunge Jimbo la Chato Kaskazini na Chato Kusini 



KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2025

 

CCM WILAYA YA CHATO IMETOA KATAZO LA MIKUTANO ISIYO RASIMI KWA WAGOMBEA UBUNGE

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita Kwa kushirikiana na Sekeretalieti ya CCM Wilaya imetoa Katazo la Mikutano isiyo Rasmi.

 

Katika hatua nyingine kamati hiyo imetoa maelekezo mbalimbali Kwa Wagombea Ubunge katika Majimbo Mawili ya Chato Kasikazini na Chato Kusini wakitakiwa kutii kanuni za Uchaguzi,kukemea Vikari Siasa za Kuchafuana Kwa lengo la Kujenga Umoja,Ushirikiano Kwa maslahi mapana ya CCM.

Akifungua kikao cha maelekezo Kwa wagombea Ubunge katika Majimbo Mawili ya Wilaya ya Chato, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chato Barnabas Nyilembe amewapongeza wagombea Kwa kujitokeza Kwa wingi katika nafasi ya Ubunge.

Kwa upande wa  jimbo la Chato Kasikazini wamejitokeza waombaji nafasi ya Ubunge 15 wakati  Jimbo la Chato Kusini wamejitokeza wagombea 18  na kusisitizwa kwa pamoja kuacha Siasa chafu za kuchafuana Kwa sababu Chama cha Mapinduzi kimejipanga kushinda Kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Aidha Nyilembe amekemea wagombea kutumia Vitendo vya rushwa kuwashawishi wajumbe ili kuwapigia Kura baada ya kuchaguliwa kwa majina matatu yatakapo pendekezwa hali hiyo haikubaliki Kwa sababu ni ukwiukwaji wa kanuni za Chama cha Mapinduzi na kwamba watakapobaini kukiuka kanuni hizo  watawajibishwa.

Amesema Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chato kimejipanga kuangalia mienendo ya Wagombea Ubunge ili kupata wagombea wenye Sifa zinazostahili kuwatumikia mwananchi pia kukiwakilisha Vema Chama hicho kwa kuonyesha tabia nzuri kwa jamii yetu ili kujenga heshima ya Wilaya ya Chato hivyo wagombea wanatakiwa kuwa waadilifu,uaminifu, wazalendo na mwenye maono mapana kwa manufaa ya Taifa.

Awali akisoma kanuni za Uchaguzi za Chama cha Mapinduzi kwa wagombea Ubunge, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chato  Charles Mazuri ametoa Katazo la Mikutano isipokuwa Rasmi kwa kuzingatia kanuni inayosema kwamba kuongoza kura siyo kigezo cha kuteuliwa hivyo atakaye fanya Makosa Chama hakitamfumbia macho na badala yake atawajibishwa.

Aidha amewataka kuacha tabia ya kujichukia Sheria mikononi endapo watabainika Changamoto Kwa wagombea na badala yake wanatakiwa kutoa Taarifa kwenye Ofisi za Chama ili taratibu za kuchukua hatua zifuatwe Kwa majibu wa kanuni zinavyo elekeza kwamba wagombea wanatakiwa kushirikiana, kujenga Urafiki,kuheshimiana na Kupendana, ili kuimarisha Umoja uliopo ndani ya CCM .

 

Mwaka 2015 katika kura za maoni wagombea Ubunge ndani ya CCM walijitokeza 47,           wakati Mwaka 2020 wagombea Ubunge walijitokeza 54 likiwa Jimbo Moja na baada ya Jimbo la Chato kugawanywa kuwa majimbo mawili Mwaka huu 2025 na kupatikana Jimbo la Chato kasikazini lenye wagombea Ubunge 15 na Chato Kusini lenye wagombea 18 hali inayotoa taswira mpya kwamba idadi ya watu kugombea mwaka huu  kupungua idadi ikilinganishwa na Mwaka 2015 na Mwaka 2020. 

Mwisho

**********


Post a Comment

0 Comments