Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amewaagiza
majaji wafawidhi wa mahakama kuu kufanya utafiti ili kubaini chanzo cha uwepo wa kesi nyingi
za mauaji katika mkoa wa Mara na za ubakaji katika mkoa wa Mwanza.
Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma ametoa maagizo hayo Jijini Mwanza wakati akifungua kikao kazi ambacho kimewakutanisha majaji wafawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania.
Aidha Jaji mkuu huyo amesema karne ya 21 ya Sayansi na Teknoljia ni muhimu ikawa ni chachu ya utoaji haki kwa wananchi wenye changamoto za kimahakama kwa kutumia mifumo ya TEHAMA.
Awali Jaji kiongozi wamahakama kuu ya Tanzania Daktari Mustapha Mohamed Siyani akitoa taarifa ya utendaji kazi amesema majaji wafawidhi wameweza kupiga hatua katika utoaji huduma kwa wananchi ikiwemo kupunguza mashauri katika mahakama zao licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali.
Mh. Mustapha Mohamed Siyani – Jaji Kiongozi mahakama
kuu ya Tanzania
Nao baadhi ya majaji wafawidhi wa mahakama kuu ambao
wameshiriki kikao kazi hicho wamesema yapo maeneo yanayotakiwa kufanyiwa
utafiti na kuahidi kuzingatia mfumo wa TEHANMA katika kutafuta
ufumbuzi wa changamoto zilizopo.
Mh.Rose Ibrahim – Jaji mfawidhi mahakama kuu
kanda ya Morogoro
Kikao kazi hicho cha siku tatu kimewashirikisha majaji
wafawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania.
Mwisho
********
0 Comments