Sengerema
Mwanza
Watendaji wa kata nchini wameshauriwa kutokiuka sheria kanuni na taratibu zilizopo na badala
yake wanapaswa kuzizingatia wanapo wahudumia wananchi katika maeneo yao.

Mkufunzi wa elimu ya Uraia na Utawala Bora kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Mrakibu masaidizi wa Polisi Iddah John ametoa Rai hiyo wakati akitoa mada ya Ulinzi na Usalama wa Nchi katika mafunzo kwa kamati ya ulinzi wilaya ya Sengerema, viongozi wa serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Buchosa mkoani Mwanza
ASP Iddah John – Mkufunzi wa mafunzo
Iddah amesema ni wajibu wa viongozi wote kufuata sheria kanuni, taratibu pamoja na miongozo iliyopo katika kuongoza.

Viongozi wa kamati ya Usalama
Katibu Tawala wa wilaya ya Sengerema Cuthbert Midala
akifungua mafunzo hayo amewasisitiza washiriki kuyatumia kwa malengo
yaliyokusudiwa kwa kutambua elimu hiyo ni muhimu.
Cuthbert Midala Katibu Tawala wilaya ya Sengerema aliyesimama
Dorice Dario ni Wakili wa serikali ambaye ni Mratibu wa
mafunzo kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ameyataja baadhi ya malengo kuwa ni Pamoja
na kuwajengea uwezo viongozi wanaosimamia serikali za mitaa, wataalam katika
Halmashauri na watendajki wa kata ili kuongoza kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, pia viongozi wa
serikali za mitaa kujengewa uwezo kuhusu wajibu Demokrasia na Utawala Bora
Dorice Dario - Mratibu wa mafunzo Wizara ya Katiba na
Sheria
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Nyehunge Judith
Mathias Pamoja na Mtendaji wa kata ya Ibisebageni Masija
Haruni ambao wameshiriki mafunzo hayo wameishukuru serikali na kusema yametolewa
kwa muda mwafaka na kuahidi Kwenda kuyatumia kikamilifu.
Judith Mathias – Mtendaji kata ya Nyehunge
Masija Hruni – Mtendaji wa kata ya Ibisebageni
Wawezeshaji wa mafunzo hayo wanatoka OR- TAMISEMI, Wizara
ya Katiba na Sheria,Wizara ya Mambo ya Ndani kutoka Polisi, Pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora na mada mbalimbali zimetolewa ikiwemo Demokrasia na Utawala Bora, Ulinzi
na Usalama wa nchi.
Mwisho
********
0 Comments