Ticker

6/recent/ticker-posts

UHABA WA MASHINE ZA KUPIMIA AFYA YA UDONGO KIKWAZO KWA WAKULIMA MAGU

Kukosekana kwa elimu ya kutosha na uhapa wa mashine za kupimia afya ya udongo kumetajwa kuwa kikwazo cha wakulima wengi kushindwa kulima kilimo cha tija Wilayani Magu mkoani Mwanza.


Hayo yamebainika katika  ziara ya madiwani, wataalam wa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza ambayo imeongozwa na kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Marco Minzi diwani wa kata ya Bukandwe.



                                            Mh. Marco Minzi – Diwani kata ya Bukandwe

Kwa upande wake Afisa kilimo  wa  wilaya ya Magu  Baguna Linus amesema kuna uhaba wa mashine ya kupimia afya ya udongo katika mashamba ya wakulima lakini  pamoja na changamoto zilizopo  ipo mikakati ya kuwanusuru wakulima hao kwa kununua mashine zingine ili kila tarafa iwe na mashine ya kupimia afya ya udongo.

 

        Baguna Linus – Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Magu

 

Ziara hiyo ya kutembelea mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Bundilya kata ya Kahangara ni sehemu ya kujifunza kwa  madiwani hao ambao wameahidi kwenda kuwasisitiza wakulima kulima kilimo cha kisasa kwa kupima afya ya udongo na kuweka mbolea.ya samadi kwenye mashamba yao.

                              Mh.Faustine John  – Diwani kata ya Kongolwa           


                                          Mh.Faustine Makioki – Diwani kata ya Sukuma

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya maendeleo ya Gavernance Links Daktari Donald Kasongi amesema ni muhimu afya ya udongo ikapimwa ili wakulima waweze kulima  kilimo chenye  tija kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.

                         

Dkt Donald Kasongi - Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Gavernance Links

 Afisa  kilimo kutoka Dacca programme TAHEA Bundala Ramadhan ametoa ushauri  kwa wakulima kutumia zaidi mbolea ya samadi kwa wakulima  huku mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Bundilya Reuben Mpugeji akieleza namna ambavyo kilimo cha kisasa cha zao la mahindi kilivyomnufaisha.

 

                       
                                Bundala Ramadhan - Afisa  kilimo kutoka Dacca programme TAHEA

 Mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Bundilya kata ya Kahangara Reuben Mpugeji amewashukuru madiwani hao hao pamoja na watalam kwa kufanya ziara katika kijiji hicho na kueleza jinsi alivyokwisha nufaika na zoezi la upimaji wa afya ya udongo ambapo kwa sasa anauwezo wakuvuna magunia kati ya 20 hadi 30 kwa hekari moja tofauti na ilivyokuwa hapo awali kuvuna maguni matano au sita.

                   

                             Reuben Mpugeji - Mkulima wa Kijiji cha Bundilya

 Wilaya ya Magu yenye kata 25, vijiji 82 na vitongoji 500 ni miongoni mwa wilaya zenye wakulima na wafugaji nchini.

Mwisho 

Post a Comment

0 Comments