Ticker

6/recent/ticker-posts

RC TABORA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI GPSA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Paul Chacha amemsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa huduma ya ununuzi serikalini GPSA wa Mkoa huo Mayala Ambuli pamoja na Watumishi Wawili wa Wakala wa Barabara Tanroads) kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.



Paull Chacha  -  Mkuu wa mkoa wa Tabora

Chacha amechukua hatua hiyo baada ya kupokea Malalamiko kutoka kwa Wateja wa GPSA Mkoani Tabora  pamoja na viongozi akiwemo yeye binafsi kuwa Muhanga wa Lugha ambazo hazina staha kutoka ndugu Mayala.

 "Leo asubuhi nimefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi ya Wakala wa huduma ya ununuzi Serikalini  GPSA Mkoa wa Tabora, nikiwa Katika ziara hiyo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora nimemsimamisha Kazi kupisha Uchunguzi ndugu Mayala Ambuli ambaye alikuwa ni Meneja wa GPSA mkoa wa Tabora kwa tuhuma za Kutumia Madaraka yake vibaya, kutoa Lugha zisizo na Staha kwa Wateja wa GPSA na Viongozi wa Serikali na kuwa na Utovu wa nidhamu Kazini"Alisema Chacha Wakati wa kikao hicho. 

 Pia, Mkuu wa Mkoa Tabora Paul Chacha amefanya ziara ya Kushtukiza katika Ofisi ya Wakala wa Barabaraba Tanzania  TANROADS  na kufanya kikao kifupi na Watumishi wa Ofisi hiyo na kumuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora Mhandisi Rafael kuwatoa watumishi wawili wa Mzani mdogo wa Tuli ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za kupokea rushwa zinazowakabili.

 Aidha Chacha amewaasa watumishi wote wa Mkoa wa Tabora, kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni ,  taratibu na misingi ya utumishi wa Umma na si vinginevyo. 

 "Amesisitiza kuwwa akiwa bado anahudumu kwa nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora hatakubali  mtu yeyote au watu wanafanya makosa hasa ya Matumizi mabaya ya madaraka kwa manufaa yao binafsi, kwamba atakuwa Mkali muda wote kwa watumishi wa aina hiyo" Alionya Chacha

 Kwa upande mwingine  Chacha amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Tabora kwa kuendelea kumpa ushirikiano ikiwemo kumpatia taarifa moja kwa moja juu ya watumishi ambao wanatumia vibaya ofisi zao au maeneo yao ya kazi na lazima hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watumishi wa aina hiyo.

Amewahakikishia na kuwaondoa hofu Wananchi kuwa watumishi wote wameletwa katika Tabora kwa ajili ya kuwatumikia na sio kutumikia madaraka yao ikiwemo  kuwaonea hivyo nilazima misingi ya Utumishi wa Umma izingatiwe ili kila mwananchi anufaike na matunda ya serikali yake  kwa kupata haki na huduma anayostahili kutoka katika sekta mbalimbali.

Mwisho

*********

Post a Comment

0 Comments