Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAWATAKA WATAALAMU WA TAASISI ZA KIFEDHA KUFANYA UTAFITI WA UWEKEZAJI

NMB YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA

Mwanza

 Serikali imewataka wataalam wa Taasisi za kifedha  kujikita katika kufanya utafiti utakaosaidia kutoa fursa  ya uwekezaji kwa vijana wanaojihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba  katika ziwa victoria ili waweze kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda  wakati akifungua  mkutano mkuu wa mwaka wa NMB  ambao umefanyika jijini Mwanza unaoenga kufanya tathimini  ya mwaka uliopita na  kuweka mikakati ya mwaka unaofuata 


                                              Said Mtanda  - Mkuu wa mkoa wa Mwanza

 Aidha Mtanda amesema  Mwanza ni habu ya kiuchumi kwa kanda ya ziwa na nchi za maziwa makuu hivyo ni muda mwafaka  kufanya uwekezaji ukiwemo  uchumi wa buluu  kwa ufugaji kwa njia ya vizimba katika ziwa Victoria.

 

                                          Said Mtanda  - Mkuu wa mkoa wa Mwanza

 Kwa upande wake  Afisa mkuu wa sekta binafsi wa NMB   Philbert  Mponzi amesema serikali imeendelea  kuweka mazingira rafiki hivyo  dhamira yao ni kuoa  huduma  bora zenye  tija zinaendelea kutolewa kwa Watanzania.

 

                                                   Philbert Mponzi - Afisa mkuu wa sekta binafsi wa NMB 

 Meneja wa NMB kanda ya ziwa Faraja Ng'ingo anaona kufanyika kwa mkutano huo ni sehemu ya mikakati inayofanywa na uongozi wa Benki hiyo  maka makuu katika kuendelea kutao huduma za kifedha kwa wateja wao.

 

                                                  Faraja Ngingo - Meneja wa NMB kanda ya ziwa

Naye meneja wa tawi la benk House  NMB kanda ya Dar es Salaam  Frednand Mpono  ameushukuru uongozi  na wkueelezea manufaa ya mkutano huo.


                                  Frednand Mpono - Meneja  NMB tawi la Benki House Dar es  Salaam

Mkutano huo ambao hufanyika kila  mwaka umeshirikisha uongozi wa NMB makao makuu, mameneja wa kanda nane za benki hiyo  matawi 241, wataalam pamoja na watumishi.

Mwisho

********

Post a Comment

0 Comments